Vipimo
1 Kikombe cha mchele.
1 Kijiko cha kulia cha unga wa ngano.
3/4-1 Kikombe cha tui la nazi zito.
2 Mayai.
1 Kijiko cha chai cha hamira.
1/2- 3/4 kikombe cha sukari.
Iliki kiasi upendacho.
Naman Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha na kuroweka mchele ndani ya maji ya baridi masaa manane au siku moja.
- Mimina vifaa vyote ispokuwa sukari, ndani ya blender na usage mpaka mchele uwe umesagika kabisa.
- Mimina sukari ndani ya mchanganyiko na usage tena kidogo tu.
- Mimina mchanganyiko ndani ya bakuli na ufinike. Weka bakuli mahali penye joto ili mchanganyiko uuumuke.
- Mchanganyiko ukisha umuka, weka karai kwenye moto.
- Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia kila kitumbua.
- Mimina mchanganyiko kiasi kwenye karai kulingana na kikarai unachotumia.
- Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
- Panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.
No comments:
Post a Comment