Vipimo
Mchele 2 Vikombe
Tui la nazi zito 2 Vikombe
Hamira 1 Kijiko Cha chai
Unga wa ngano 2 vijiko vya supu
Iliki kiasi upendavyo
Sukari kiasi upendavyo
Yai 1
Vipimo Vya Tui La Kupaka
Tui la nazi 2 Vikombe
Iliki ya unga Kiasi upendacho
Sukari Kiasi upendacho
Unga wa ngano 1 kijiko cha supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Changanya vitu vyote vya tui la kupaka katika kisufuria kidogo.
2. Lipike tui huku walikoroga mpaka lichemke na liwe zito.
3· Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
4· Mimina vifaa vyote isipokuwa yai na sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
5. Mimina sukari na yai usage kidogo tu kiasi cha kuchanganya.
6· Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
7· Ukishafura , weka chuma kipate moto. (Ni bora kutumia kichuma kidogo)
8.Katika sahani ya kupakulia, paka tui kote.
9· Tia kijiko nusu cha chai cha mafuta au samli kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko ukitumia upawa na ufunike.
10· Kibibi kikianza kuiva na kushikana upande mmoja , kigeuze upande wa pili mpaka kigeuke rangi na kuiva.
11. Panga kwenye sahani iliyopakwa tui.
12· Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; kila ukiepua kibibi, panga juu ya mwenzake kama ilivyo kwenye picha na upake tui juu yake.
No comments:
Post a Comment