Vipimo:
Unga 2 vikombe vya chai
Sukari 1 ½ kikombe cha chai
Mafuta 1 ½ kikombe cha chai
Baking powder 2 vijiko vya chai
Siagi ¼ kikombe cha chai
Mayai 6
Sukari ya hudhurungi (brown) 1 ¾ kikombe cha chai
Manasi ya kopo yaliyokatwa duara 1 kopo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Unayeyusha sukari ya hudhurungi pamoja na siagi. Ikishayeyuka vizuri unamimina kwenye sufuria au trei ya kuchomea keki.
2. Panga vipande vya nanasi kwenye hiyo sufuria/trei. Weka pembeni. Ukipenda katikati ya duara ndogo ya nanasi weka cheri moja.
3. Kwenye bakuli la kuchanganyia keki la mashine, piga mayai, sukari, vanilla mpaka iwe kama malai (crème) na nzito.
4. Mimina unga pamoja na baking powder, piga kidogo, mwisho mimina mafuta.
5. Mimina huo mchanganyiko kwenye sufuria/trei uliyopanga vipande vya nanasi, tayari kuchoma.
6. Weka moto 180 C choma kwa muda wa dakika 30 – 35.
7. Ikishaiva, acha ipowe kwa muda wa dakika 7, mimina chini juu kwenya sahani, tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment