Saturday, February 18, 2012

Samaki wa Lax kwenye oven


Mchukue lax akiwa pamoja na ng'ozi yake
vitu vinavyohitajika ni
Ndimu ya pilipili ( lemon pepper, citronpeppar)
 binzari kavu  ( dried dill, torkad dill)
maganda ya limao (grated lemon peel, rivet cintronskal)
Chumvi ya mawe ( coarse salt, grovsalt)


Chukua chombo utakachopikia weka chumvi ya mawe sehemu yote,
halafu mchukue lax umuweke juu ng'ozi ya ikiwa chini.
mpake binzari kavu na maganda ya limao pamoja na ndimu ya pili pili, ukitaka chumvi kdg.













Mtie kwenye oven moto 200c kwa dakika 20-30 angalia mara kwa mara na uma kama imeiva
Usiiache sana mpaka ikakauka haito kuwa nzuri.






Unaweza kumla na sosi yeyote ya samaki utakayopenda na saladi pia, Enjoy.


 samahani kama takua nimekosea majina ya viungo kwa kiswahili ila nimeweka kwa kiswidi na kiingereza.



No comments:

Post a Comment