VIPIMO
Mchele Basmati Mugs 2 ½
Vitunguu (Vikubwa kiasi) 3
Tuna Vibati 3
Carrot 2 kubwa
Tomatoe paste 1 kikop
Thomu 2 Vijiko vya supu
Tangawizi 2 Vijiko vya supu
Uzile (Bizari ya pilau ya unga) (cummin powder )
(Jeera) ½ Kijiko cha supu
Mdalasini ½ Kijiko Cha supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Tuna carrots (grate) ziwe kama chicha weka kando.
2. Kaanga vitunguu 2 mpaka viwe brown weka pembeni.
3. Kaanga Kitunguu cha 3 halafu changanya na tangawizi, thomu, na tuna huku unakoroga.
4. Changanya
na tomatoe, uzile (cummin powder) na mdalasini, koroga vizuri
(hakikisha umeweka mtoto mdogo mdogo kwani ni rahisi kuungua)
5. Ikiwiva epua weka pembeni.
6. Chemsha wali wako kwa maji mengi na uuchuje kabla haujawiva vizuri na uugawe sehemu 4.
7. Chukua
trey au sufuria ambayo itaweza kuingia vitu vyote uilivyoandaa, tandaza
fungu la kwanza la wali halafu utandaze carrot juu yake.
8. Tandaza fungu la pili la wali halafu utandaze vitunguu juu yake.
9. Tandaza fungu la tatu la wali halafu utandze tuna (masalo) juu yake.
10. Mwisho tandaza fungu la nne la wali, ufunike vizuri na upike kwenye overn (bake) 350 Deg C kwa muda wa dakika 20
No comments:
Post a Comment