vipimo
Viazi (mbatata) 2
Kamba 1 Lb
Vitunguu 2
Nyanya 2
Pilipili hoho (green pepper) 1
Thomu 1 kijiko cha chai
Tangawizi 1 kijiko cha chai
Uzile (bizari ya pilau ya unga-Jiyra) ½ kijiko cha chai
Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Pilipili ya unga ½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo ½ kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha
1) Changanya kamba na thomu, tangawizi, pilipili manga, pilipili ya unga, jira na chumvi.
2) Katakata vitunguu weka pembeni.
3) Katakata pilipili hoho weka pembeni.
4) Katakata Nyanya weka pembeni.
5) Menya viazi na uvikate vidogo vidogo.
Namna Ya Kupika
1) Kaanga kamba mpaka wabadilike rangi, watie kwenye bakuli.
2) Kaanga viazi mpaka viwive na vibadilike rangi, vitoe, mimina kwenye bakuli.
3) Kaanga pilipili hoho viwive na vibadilike rangi, vitoe.
4) Kaanga vitunguu mpaka vibadilike rangi, mimina nyaya kaanga pamoja, kisha tia nyanya ya kopo na chumvi.
5) Endelea kukoroga.
6) Mimina maji kama robo kikombe, ukishawiva vizuri, mimina katika bakuli la mchanganyiko na ukoroge kidogo ili vichanganyike tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment