Saturday, February 18, 2012

Viazi Vya Nazi Kwa Nyama




Vipimo


Viazi                               3lb

Nyama                           1lb

Kitunguu                        1

Nyanya                          2

Thomu                          1 kijiko cha chai

Manjano                        ½ kijiko cha chai

Curry powder                ½ kijiko chai

Nyanya kopo                  1 kijiko cha chai

Pilipili ya unga                  kiasi upendavyo

Chumvi                           kiasi

Kidonge cha supu             1

Tui la nazi                       1 kopoau zaidi

Mtindi ukipenda              3 vijiko vya supu

Kotmiri                           kiasi ya kupambia

Nazi ya unga                  4 vijiko vya supu

Mafuta                           2 vijiko vya supu


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika


  1. Kata nyama vipande vipande kisha chemsha na chumvi mpaka iive.
  2. Menya maganda viazi na ukate slice kubwa weka pembeni
  3. Kata kata kitunguu kisha kaanga na mafuta mpaka vibadilike rangi
  4. Tia thomu, bizari ya manjano, pilipili ya unga, nyanya kopo
  5. Kata kata nyanya nzima vipande vidogo tia na kidonge cha supu.
  6. Kisha tia viazi, nyama na tui la nazi finika mpaka viazi viwive lakini    visiwe vikavu.
  7. Tia mtindi na nazi ya unga kama vijiko 4 vya supu iache motoni kidogo kisha pakua, tupia kotmiri juu na itakuwa tayari kuliwa.. 

No comments:

Post a Comment