Vipimo
Unga 2 Vikombe
Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu
Maziwa ¾ Kikombe
Iliki Kiasi
Mafuta ya kukarangia Kiasi
Shira
Sukari 1 Kikombe
Maji ¾ Kikombe
Vanila ½ Kijiko cha chai
Zafarani (ukipenda) Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.
- Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.
- Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.
- Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha.
- Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
- Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.
- Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.
No comments:
Post a Comment