Wednesday, March 28, 2012

Viazi Vyekundu




Vipimo

Viazi /mbatata                                                       10 kiasi

Kitunguu maji kilichosagwa                                     1

Thomu iliyosagwa                                                  1 kijiko cha supu

Pilipili iliyosagwa                                                     1 kijiko cha chai

Rai (mustard seeds)                                               1 kijiko cha supu

Majani ya mchuzi (curry leaves)                             7 majani

Uwatu uliosagwa (methi)                                       1 kijiko cha chai

Nyanya kopo                                                         5 vijiko vya supu

Ndimu                                                                    3 vijiko vya supu

Mafuta                                                                   ¼ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha viazi kiasi viwive lakini  visivurugike
  2. Menya, katakata vipande weka kando.
  3. Tia mafuta katika sufuria, yakishika moto tia rai, zikaange kwa muda wa dakika moja hadi zigeuke rangi kidogo.
  4. Tia majani ya mchuzi, uwatu, thomu, kitunguu maji, pilipili  kaanga kidogo tena.
  5. Tia nyanya kopo endelea kukaanga kidogo kisha tia chumvi, ndimu na maji kiasi kidogo ili kufanya rojo kiasi.
  6. Mimina viazi, changanya, pakua katika sahani.

Pizza Ya Samaki



Vipimo

Tuna steki wa kopo (oiled)                                        180 – 185 g 

Tomato ya kopo(paste)                                            3 Vijiko vya supu

Kitunguu maji                                                           1

Chumvi                                                                    1 kijiko cha chai

Unga wa ngano                                                        4 vikombe

Mafuta ya zaituni                                                      Nusu kikombe

Hamira                                                                    1 kijiko cha chai

Cheese ya Pizza                                                        100 g



Namna Ya Kutayarisha Na Kupika


  1. Katika bakuli kubwa tia unga, hamira,mafuta na chumvi.Kisha mimina maji kidogo kidogo hadi mchanganyiko uwe donge la kunata kiasi tu. 
  2. Funika na uwache unga kwa muda wa nusu saa kisha ukande tena kiasi ukijipaka mafuta mikononi, ufinike kwa muda wa  masaa manne hadi sita.
  3. Ukishaumuka kufura itakuwa tayari kwa kuandalia vitu vya kuweka juu.
  4. Mimina tuna kwenye sahani huku ukichambua kuzidisha vijipande pande.
  5. Katakata kitunguu slesi nyembamba kando, tomato (paste) ndani ya kijibakuli tia maji vijiko 2 vya supu kisha koroga ili iwe kidogo nyepesi.
  6. Pake siagi au mafuta kiasi katika treya utakayochomea.
  7. Chukuwa unga ulioumuka ukande ufanye donge moja  na limwagie unga mkavu.
  8. Litandaze donge kwenye treya mpaka upate chapati kubwa kwa mikono bila kutumia kifimbo.
  9. Mwagia tomato (paste) kwenye pizza utandaze ,kisha  tuna halafu tupia vitunguu na utamalizia na  cheese.  
  10. Choma  kwenye oveni kwa moto wa 200°C  kwa muda wa dakika  25. Kisha unaweza kukata (shape) upendayo na itakuwa tayari kuliwa.

Kidokezo:

 Ukipenda  pilipili za kuwasha unaweza kuongezea na pia unaweza kutumia brokoli badala ya tuna.Ni vizuri kuliwa ikiwa moto moto.  

Monday, March 5, 2012

Biskuti Za Kuchoveya Chokoleti

 

 

 

Vipimo:


Unga                                                            300gm
Siagi                                                            225gm
Icing Sugar                                                  60gm
Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate)             225gm
Vanilla                                                          2 kijiko cha chai
Yai                                                               1  
Baking Powder                                              ½  kijiko cha chai
Njugu za vipande                                           ½  kikombe cha chai
Njugu zilizosagwa                                        ¼  kikombe cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 
1.       Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini
2.       Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri
3.       Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike.
4.       Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k)
5.       Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350°C , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe
6.       Yayusha chokoleti  tia kwenye bakuli ndogo.
7.       kisha paka kwa kijiko au chovyea upande  mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga.
8.       Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.

 Kidokezo:
Njugu aina yoyote upendazo, njugu za kawaida, au jozi (walnut), lozi (almond)  au pistachio.

Visheti



Vipimo


Unga                                                   2 Vikombe

Samli au shortening ya mboga              2 Vijiko vya supu

Maziwa                                               ¾ Kikombe

Iliki                                                      Kiasi

Mafuta ya kukarangia                          Kiasi



Shira


Sukari                                 1 Kikombe

Maji                                    ¾ Kikombe

Vanila                                 ½ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda)             Kiasi



Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.
  2. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.
  3. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.
  4. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha.
  5. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
  6. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.
  7. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

Labania Za Maziwa


*Vipimo




Maziwa ya unga                 2 vikombe

Sukari                               3 vikombe

Maji                                  3 vikombe

Unga wa ngano                  ½ kikombe

Mafuta                             ½ kikombe

Iliki                                   kiasi


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika


  1. Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania
    Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri 
  2. Kisha mimina  mafuta koroga 
  3. Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka 
  4. Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya  browni isiokoleza. 
  5. Kisha mimina  mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe  na kata kata upendavo na itakuwa tayari.

* Katika vipimo ni vizuri utumie kikombe cha kupimia (measuring cup)